Mafia wa Black Axe wa Nigeria wapata 'pigo kubwa' kutoka kwa Interpol - BBC News Swahili (2024)

Mafia wa Black Axe wa Nigeria wapata 'pigo kubwa' kutoka kwa Interpol - BBC News Swahili (1)

Chanzo cha picha, Interpol

Maelezo kuhusu taarifa
  • Author, Charlie Northcott
  • Nafasi, BBC Africa Eye

Vitengo vya polisi kote duniani vimeungana katika msururu wa operesheni za siri zinazolenga mojawapo ya mtandao unaoogopwa zaidi wa uhalifu Afrika Magharibi - Black Axe.

Operesheni kwa jina Jackal III ilishuhudia maafisa waliovaa nguo maalum zinazovaliwa na polisi au wanajeshi kwa ajili ya ulinzi katika nchi 21 kati ya Aprili na Julai 2024.

Operesheni hiyo iliyoratibiwa na shirika la polisi wa kimataifa Interpol, ilisababisha kukamatwa kwa watu 300 wenye uhusiano na mtandao wa Black Axe na makundi mengine tanzu.

Interpol iliita operesheni hiyo "pigo kubwa" kwa mtandao wa uhalifu wa Nigeria, lakini ilionya kwamba kufikia kwake kimataifa na ustadi wa teknolojia unamaanisha kuwa bado ni tishio la kimataifa.

Pia unaweza kusoma:

Kwa mfano, mamlaka za Canada zilisema walivamia mpango wa utakatishaji fedha unaohusishwa na Black Axe wenye thamani ya zaidi ya $5bn (£3.8bn) mwaka wa 2017.

"Wamejipanga sana na wako makini kweli," Tomonobu Kaya, afisa mkuu wa Kituo cha Uhalifu wa Kifedha na Kupambana na Ufisadi cha Interpol, aliiambia BBC.

Kulingana na ripoti ya 2022 ya Interpol, "Black Axe na vikundi sawia na hicho vinahusika na ulaghai mwingi wa kifedha duniani".

Bw Kaya alisema ubunifu katika programu za kutuma pesa na sarafu za kidijitali vinafikiwa na kundi hilo, ambalo linajulikana kwa ulaghai wa mtandaoni wa mamilioni ya dola.

"Makundi haya ya wahalifu ni watumiaji wa awali wa teknolojia mpya… Maendeleo mengi ya kiteknolojia yanafanya iwe rahisi sana kuhamisha pesa ulimwenguni kote kinyume cha sheria," alisema.

Operesheni Jackal III ilikuwa ikifanywa kwa miaka mingi na kupelekea kunaswa kwa mali haramu ya $3m na zaidi ya akaunti 700 za benki kufungwa.

Wanachama wengi wa Black Axe wamesoma hadi chuo kikuu na huajiriwa wakati wakiwa bado shuleni.

Shirika hilo ni mtandao wa siri wa uhalifu wenye shughuli za usafirishaji haramu, ukahaba na mauaji kote ulimwenguni.

Uhalifu wa mtandaoni, unaolenga watu binafsi na biashara, ndio chanzo kikuu cha mapato cha mtandao huo.

Operesheni nyingi za polisi zinazoitwa "Jackal" zimefanyika tangu 2022.

Makumi ya wanachama wa Black Axe na magenge mengine wamekamatwa na vifaa vyao vya kielektroniki kunaswa wakati wa uvamizi huu wa kimataifa.

Waliofanikiwa kugundua katika operesheni hii, kumewezesha Interpol kuunda hifadhidata kubwa ya kijasusi, ambayo sasa inashirikishwa maafisa katika nchi zake zote 196 wanachama.

"Tunahitaji kuwa na data na kukusanya matokeo yetu kutoka kwa nchi hizi ili kusaidia kujenga taswira ya njia za uendeshaji shughuli zao," alisema Bw Kaya.

Mafia wa Black Axe wa Nigeria wapata 'pigo kubwa' kutoka kwa Interpol - BBC News Swahili (2)

Chanzo cha picha, Interpol

Licha ya wahalifu kukamatwa mara nyingi kimataifa, baadhi ya wataalam wanahisi hatua zinazochukuliwa dhidi yao hazitoshi kukabiliana na mizizi ya makundi haya ya uhalifu Afrika Magharibi.

"Msisitizo lazima uwe katika kuzuia si kwa operesheni za moja kwa moja dhidi ya vikundi hivi vya uhalifu," alisema Dk Oluwole Ojewale, Mratibu wa Kanda ya Afrika Magharibi kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Usalama.

Nigeria, ambayo imeshuhudia maandamano makubwa ya kupinga ŕushwa katika wiki za hivi majuzi, ni moja ya mataifa yenye uchumi mkubwa zaidi baŕani Afŕika, lakini ina hadi watu milioni 87 wanaoishi katika lindi la umaskini, kulingana na Benki ya Dunia.

Pia ni eneo kuu la usajili wa wanachama wa kundi la Black Axe.

Interpol ilisema inafanya mazoezi na washika wadau wakuu wa Nigeria na maafisa wa polisi. Lakini rushwa, na madai ya ushirikiano kati ya kundi la Black Axe na mamlaka za mitaa, bado ni kikwazo kikubwa.

"Ni wanasiasa ambao wanawapa wavulana hawa silaha," alisema Dkt Ojewale. "Kwa jumla, kushindwa kwa utawala nchini kumekuwa chachu ya wavulana hawa kujiunga na kundi la [Black Axe]."

Licha kufanyika kimataifa, chimbuko la operesheni za Interpol za Jackal ni Ireland.

Kufuatia msururu wa uvamizi wa polisi uliofanywa na Taasisi ya Kitaifa ya Uhalifu wa Kiuchumi ya Garda mnamo mwaka 2020, wanachama wachache wa Black Axe walikamatwa, na kuwa mwanga katika ufichuzi wa mtandao huu mpana zaidi wa uhalifu.

"Kiwango cha shughuli za utakatishaji fedha huko Ireland kilikuwa cha juu," aliongeza.

Mafia wa Black Axe wa Nigeria wapata 'pigo kubwa' kutoka kwa Interpol - BBC News Swahili (3)

Chanzo cha picha, Interpol

Baadaye, polisi walitambua watu 1,000 waliokuwa na uhusiano na kundi la Black Axe nchini Ireland na wamekamata mamia ya watu kwa ulaghai na uhalifu wa mtandaoni.

"Uwizi wa benki sasa unafanywa kwa kipakatalishi - ni wa kisasa zaidi," alisema Det Supt Cryan.

Anakadiria €200m ($220m; £170m) zimeibiwa mtandaoni nchini Ireland katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, na kwamba ni asilimia 20 pekee ya uhalifu wa mtandaoni ambao unaaminika kuripotiwa.

"Huu sio uhalifu wa kipekee au wa kawaida ... Watu wanaofanya maamuzi wanahitaji kujua jinsi hali hii ilivyo mbaya," alisema.

Interpol imetumia teknolojia yake mpya katika jaribio la kukabiliana na ubunifu huu wa teknolojia, na kuzindua mfumo wa malipo Duniani unaojulikana kama Global Rapid Intervention of Payments (I-GRIP).

Utaratibu huo, unaowezesha mamlaka katika nchi wanachama kufungia akaunti za benki duniani kote kwa kasi isiyokuwa na kifani, ulitumiwa kusitisha kashfa ya $40m iliyolenga biashara ya Singapore mwezi uliopita.

Bw Kaya wa Interpol alisema teknolojia kama hii itafanya iwe vigumu kwa wahalifu kusafirisha pesa kuvuka mipaka bila kukamatwa na kuadhibiwa.

Juhudi zinaendelea kukusanya na kushirikisha taarifa za kijasusi kuhusu kundi la Black Axe na makundi mengine ya Afrika Magharibi na polisi duniani kote.

"Ikiwa tunaweza kukusanya data hizi tunaweza kuchukua hatua," alisema.

Pia unaweza kusoma:
  • Tapeli wa mapenzi alivyowalaghai wanawake pauni 80,000

  • 'Kupewa dawa za kulevya, kuibiwa, kuuawa': Jiji linalonasa watalii wa Marekani katika mtego wa programu za kuchumbiana

  • Utapeli wa ustadi wa juu duniani unaojumuisha Wanigeria kwa kuzimiwa simu tu

Imetafsiriwa na Asha Juma

Mafia wa Black Axe wa Nigeria wapata 'pigo kubwa' kutoka kwa Interpol - BBC News Swahili (2024)
Top Articles
Tower Of Trample Walkthrough
Report: Haunted Mansion Secretly Being Changed To Avoid Offending Disney Park Guests - Inside the Magic
Spasa Parish
Happel Real Estate
Social Security Administration Lawton Photos
Her Triplet Alphas Chapter 32
Tripadvisor London Forum
Luxiconic Nails
Ess Compass Associate Portal Login
Denman Promo Code
Www.citizen-Times.com Obituaries
Order Irs Tax Forms Online
Step 2 Score Release Thread
What does JOI mean? JOI Definition. Meaning of JOI. OnlineSlangDictionary.com
Rebecca Benedict Forum
What Is a Food Bowl and Why Are They So Popular?
James Cameron And Getting Trapped Inside Your Most Successful Creation
2887 Royce Road Varysburg Ny 14167
Gargoyle Name Generator
Ups Customer Center Locations
How Much Is Felipe Valls Worth
Water Leaks in Your Car When It Rains? Common Causes & Fixes
Learning Channel Senior Living
Jordan Torres Leaked
Zillow Group, Inc. Aktie (A14NX6) - Kurs Nasdaq - MarketScreener
Mapa i lokalizacja NPC w Graveyard Keeper - Graveyard Keeper - poradnik do gry | GRYOnline.pl
Christian Horner: Red Bull team principal to remain in role after investigation into alleged inappropriate behaviour
How To Pause Tamagotchi Gen 2
Cronología De Chelsea Contra Fulham
Xdm16Bt Manual
Brublackvip
How to Choose Where to Stay When You Visit Pittsburgh
Mycourses Wcc
The Whale Showtimes Near Cinépolis Vista
Nina Volyanksa
Ups Store.near Me
Uc Davis Tech Management Minor
Lactobacillus reuteri : présentation, bienfaits et avis sur ce probiotique
Incident Manager (POS & Kiosk) job in Chicago, IL with McDonald's - Corporate
Vitamin-K-Lebensmittel – diese enthalten am meisten! | eatbetter: gesunde, einfache Rezepte & Tipps für jeden Tag
Ccga Address
Left Periprosthetic Femur Fracture Icd 10
Ucla Outlook Web Access
Maria Butina Bikini
100.2华氏度是多少摄氏度
Watch Races - Woodbine Racetrack
Kirstin Kresse
Osrs Nex Mass
Fast X Showtimes Near Regal Spartan
The Crew 2 Cheats für PS4, Xbox One und PC ▷➡️
Rubrankings Austin
Opsahl Kostel Funeral Home & Crematory Yankton
Latest Posts
Article information

Author: Francesca Jacobs Ret

Last Updated:

Views: 5665

Rating: 4.8 / 5 (68 voted)

Reviews: 91% of readers found this page helpful

Author information

Name: Francesca Jacobs Ret

Birthday: 1996-12-09

Address: Apt. 141 1406 Mitch Summit, New Teganshire, UT 82655-0699

Phone: +2296092334654

Job: Technology Architect

Hobby: Snowboarding, Scouting, Foreign language learning, Dowsing, Baton twirling, Sculpting, Cabaret

Introduction: My name is Francesca Jacobs Ret, I am a innocent, super, beautiful, charming, lucky, gentle, clever person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.